Zaburi15

Kitu Mwenyezi Mungu anachotaka

Zaburi ya Daudi.

1Mwenyezi Mungu, ni nani awezaye kukaakatika Hekalu lako?Nani awezaye kuishikatika mlima wako mtakatifu?
2Ni yule aendaye pasipo mawaa,atendaye yaliyo haki,asemaye kweli toka moyoni mwake,3na hana masingizio ulimini mwake,asiyemtenda jirani yake vibaya,na asiyemsingizia mwenzake,4ambaye humdharau mtu mbaya,lakini huwaheshimu wale wamwogopao Mwenyezi Mungu,yule atunzaye kiapo chakehata kama anaumia.5Yeye akopeshaye fedha yake bila riba,na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.Mtu afanyaye hayakamwe hatatikisika.