Zaburi16swh_onmm

Sala ya matumaini

Utenzi wa Daudi.

1Ee Mungu, uniweke salama,kwa maana kwako nimekimbilia.
2Nilimwambia Mwenyezi Mungu, “Wewe ndiwe Bwana wangu;pasipo wewe sina jambo jema.”3Kuhusu watakatifu walio duniani,hao ndio wenye fahari,na ninapendezwa nao.4Huzuni itaongezeka kwa walewanaokimbilia miungu mingine.Sitazimimina sadaka za damu kwa miungu kama hiyo,au kutaja majina yao mdomoni mwangu.
5Mwenyezi Mungu umeniwekea fungu langu na kikombe changu;umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.6Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri,hakika nimepata urithi mzuri.
7Nitamsifu Mwenyezi Mungu ambaye hunishauri,hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.8Nimemweka Mwenyezi Mungu mbele yangu daima.Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,sitatikisika.
9Kwa hiyo moyo wangu unafurahia,na ulimi wangu unashangilia;mwili wangu naoutapumzika salama,10kwa maana hutaniacha Kuzimu ,wala hutamwacha Mtakatifu Wakokuona uharibifu.11Umenijulisha njia ya uzima;utanijaza na furaha mbele zako,pamoja na furaha ya milelekatika mkono wako wa kuume.