Zaburi14swh_onmm

Uovu wa wanadamu

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1Mpumbavu anasema moyoni mwake,“Hakuna Mungu.”Wamepotoka, matendo yao ni maovu kabisa;hakuna hata mmoja atendaye mema.
2Mwenyezi Mungu anawachungulia wanadamukutoka mbinguniaone kama kuna mwenye hekima,yeyote anayemtafuta Mungu.3Wote wamepotoka,wote wameoza pamoja;hakuna atendaye mema,naam, hakuna hata mmoja!
4Je, watendao maovu kamwe hawatajifunza:wale ambao huwala watu wangukama watu walavyo mkate,hao ambao hawamwiti Mwenyezi Mungu?5Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu,maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.6Ninyi watenda maovu mnakwamisha mipango ya maskini,bali Mwenyezi Mungu ndiye kimbilio lao.
7Laiti wokovu wa Israeliungekuja kutoka Sayuni!Mwenyezi Mungu anaporejeshawafungwa wa watu wake,Yakobo na ashangilie,Israeli na afurahi!