Zaburi127

Bila Mwenyezi Mungu, kazi ya mwanadamu haifai

Wimbo wa kwenda juu. Wa Sulemani.

1Mwenyezi Mungu asipoijenga nyumba,wajengao hufanya kazi bure.Mwenyezi Mungu asipoulinda mji,walinzi wakesha bure.2Mnajisumbua bure kuamka mapemana kuchelewa kulala,mkitaabikia chakula:kwa maana yeye huwapa usingizi wapendwa wake.
3Watoto ni urithi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu,uzao ni zawadi kutoka kwake.4Kama mishale mikononi mwa shujaandivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.5Heri mtu ambaye podo lakelimejazwa nao.Hawataaibishwa wanaposhindanana adui zao langoni.