Zaburi128swh_onmm
Thawabu ya kumtii Mwenyezi Mungu
Wimbo wa kwenda juu.
1Heri wale wote wamchao Mwenyezi Mungu,wanaoenda katika njia zake.2Utakula matunda ya kazi yako;baraka na mafanikio vitakuwa vyako.3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaaondani ya nyumba yako;wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeitunikuizunguka meza yako.4Hivyo ndivyo atakavyobarikiwamtu amchaye Mwenyezi Mungu.5Mwenyezi Mungu na akubariki kutoka Sayunisiku zote za maisha yako,na uone mafanikio ya Yerusalemu,6nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako.Amani iwe juu ya Israeli.