Zaburi126swh_onmm

Kurejeshwa kutoka uhamisho

Wimbo wa kwenda juu.

1Mwenyezi Mungu alipowarejesha mateka Sayuni,tulikuwa kama watu walioota ndoto.2Vinywa vyetu vilijaa kicheko,ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,“Mwenyezi Mungu amewatendea mambo makuu.”3Mwenyezi Mungu ametutendea mambo makuu,nasi tumejaa furaha.
4Ee Mwenyezi Mungu, turejeshee watu wetu waliotekwa,kama vijito katika Negebu.5Wapandao kwa machoziwatavuna kwa nyimbo za shangwe.6Yeye azichukuaye mbegu zakekwenda kupanda, huku akilia,atarudi kwa nyimbo za shangwe,akichukua miganda ya mavuno yake.