Sefania3

Maisha ya baadaye ya Yerusalemu

Hatima ya Yerusalemu

1Ole mji wa wadhalimu,waasi na waliotiwa unajisi!2Hautii mtu yeyote,haukubali maonyo.Haumtumaini Mwenyezi Mungu,haukaribii karibu na Mungu wake.3Maafisa wake ni simba wanaonguruma,watawala wake ni mbwa-mwitu wa jioni,ambao hawabakizi chochotekwa ajili ya asubuhi.4Manabii wake ni wenye kiburi,ni wadanganyifu.Makuhani wake hunajisi patakatifuna kuihalifu sheria.5Mwenyezi Mungu aliye ndani yake ni mwenye haki,hafanyi kosa.Asubuhi kwa asubuhi hutoa haki yake,kila kukipambazuka huitimiza,bali mtu dhalimu hana aibu.

Yerusalemu yakataa kutubu

6“Nimeyaangamiza mataifa,ngome zao zimebomolewa.Nimeziacha barabara ukiwa,hakuna anayepita humo.Miji yao imeharibiwa;hakuna mmoja atakayeachwa:hakuna hata mmoja.7Niliuambia huo mji,‘Hakika utaniogopa na kukubali maonyo!’Ndipo makao yake hayatafutiliwa mbali,wala adhabu zangu zote hazitakuja juu yake.Lakini walikuwa bado na shaukukutenda kwa upotovu katika yote waliyofanya.”8Mwenyezi Mungu anasema,“Kwa hiyo ningojee mimi,siku nitakayosimama kuteka nyara.Nimeamua kukusanya mataifa,kukusanya falmena kumimina ghadhabu yangu juu yao,hasira yangu kali yote.Dunia yote itateketezwakwa moto wa hasira yangu yenye wivu.

Mabaki ya Israeli kurejeshwa

9“Ndipo nitatakasa midomo ya mataifa,kwamba wote waweze kuliitia jina la Mwenyezi Munguna kumtumikia kwa pamoja.10Kutoka ng’ambo ya mito ya Kushiwatu wangu wanaoniabudu,watu wangu waliotawanyika,wataniletea sadaka.11Siku hiyo hutaaibishwakwa ajili ya makosa yote uliyonitendea,kwa sababu nitawaondoa kutoka mji huuwale wote wanaoshangiliakatika kiburi chao.Kamwe hutajivuna tenakatika kilima changu kitakatifu.12Lakini nitakuachia ndani yakowapole na wanyenyekevu,ambao wanatumaini jina la Mwenyezi Mungu.13Mabaki ya Israeli hayatafanya kosa;hawatasema uongo,wala udanganyifu hautakuwakatika vinywa vyao.Watakula na kulalawala hakuna yeyoteatakayewaogopesha.”
14Imba, ee Binti Sayuni;paza sauti, ee Israeli!Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote,ee Binti Yerusalemu!15Mwenyezi Mungu amekuondolea adhabu yako,amewarudisha nyuma adui zako.Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Israeli, yu pamoja nawe;kamwe hutaogopa tena madhara yoyote.16Katika siku hiyo watauambia Yerusalemu,“Usiogope, ee Sayuni;usiiache mikono yako ilegee.17Mwenyezi Mungu, Mungu wako, yu pamoja nawe,yeye ni Shujaa mwenye nguvu anayeokoa.Atakufurahia kwa furaha kubwa,atakutuliza kwa pendo lake,atakufurahia kwa kuimba.”
18“Huzuni katika sikukuu zilizoamriwanitaziondoa kwenu;hizo ni mzigo na fedheha kwenu.19Wakati huo nitawaadhibuwote waliokudhulumu;nitaokoa vilema na kukusanyawale waliotawanywa.Nitawapa sifa na heshimakatika kila nchi ambayo waliaibishwa.20Wakati huo nitawakusanya;wakati huo nitawaleta nyumbani.Nitawapa sifa na heshimamiongoni mwa mataifa yote ya duniawakati nitakapowarudishia mateka yenumbele ya macho yenu hasa,”asema Mwenyezi Mungu.