1Kusanyikeni pamoja, kusanyikeni pamoja,enyi taifa lisilo na aibu,2kabla wakati ulioamriwa haujafikana siku ile inayopeperusha kama makapi,kabla hasira kali ya Mwenyezi Mungu haijaja juu yenu,kabla siku ya ghadhabu ya Mwenyezi Munguhaijaja juu yenu.3Mtafuteni Mwenyezi Mungu, enyi nyote wanyenyekevu wa nchi,ninyi ambao hufanya lile analoamuru.Tafuteni haki, tafuteni unyenyekevu;labda mtahifadhiwasiku ya hasira ya Mwenyezi Mungu.
Dhidi ya Ufilisti
4Gaza utaachwana Ashkeloni utaachwa magofu.Wakati wa adhuhuri Ashdodi utaachwa mtupu,na Ekroni utang’olewa.5Ole wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari,enyi Wakerethi;neno la Mwenyezi Mungu liko dhidi yenu,ee Kanaani, nchi ya Wafilisti.“Mimi nitawaangamiza,na hakuna atakayebaki.”6Nchi iliyo karibu na bahari itakuwa malishoyenye visima vya wachungaji,na mazizi ya kondoo.7Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda,hapo watapata malisho.Wakati wa jioni watajilaza chinikatika nyumba za Ashkeloni.Mwenyezi Mungu, Mungu wao, atawatunza,naye atawarudishia wafungwa wao.
Dhidi ya Moabu na Amoni
8“Nimeyasikia matukano ya Moabunazo dhihaka za Waamoni,ambao waliwatukana watu wanguna kutoa vitisho dhidi ya nchi yao.9Hakika, kama niishivyo,”asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni,Mungu wa Israeli,“hakika Moabu itakuwa kama Sodoma,Waamoni kama Gomora:mahali pa magugu na mashimo ya chumvi,nchi ya ukiwa milele.Mabaki ya watu wangu watawateka nyara;mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”10Hiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi chao,kwa kutukana na kudhihakiwatu wa Mwenyezi Mungu,Mungu wa majeshi ya mbinguni.11Mwenyezi Mungu atakuwa wa kuhofisha kwaoatakapoangamiza miungu yote ya nchi.Mataifa katika kila pwani yatamwabudu,kila moja katika nchi yake.
Dhidi ya Kushi
12“Ninyi pia, ee Wakushi,mtauawa kwa upanga wangu.”
Dhidi ya Ashuru
13Mungu atanyoosha mkono wake dhidi ya kaskazinina kuangamiza Waashuru,akiiacha Ninawi ukiwana pakame kama jangwa.14Makundi ya kondoo na ng’ombe yatajilaza pale,viumbe vya kila aina.Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembambawataishi juu ya nguzo zake.Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani,kifusi kitakuwa milangoni,boriti za mwerezi zitaachwa wazi.15Huu ndio mji uliotukuka na kuishi kwa furahawakijisikia salama.Ulisema moyoni mwako,“Mimi ndimi, na wala hapana mwingine ila mimi.”Jinsi gani umekuwa gofu,mahali pa kulala wanyama pori!Wote wanaopita kando yake wanauzomeana kutikisa mkono kwa dharau.