Zaburi133swh_onmm

Sifa za pendo la undugu

Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendezandugu wanapoishi pamoja katika umoja!2Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,yakitiririka kwenye ndevu,yakitiririka kwenye ndevu za Haruni,hadi kwenye upindo wa mavazi yake.3Ni kama umande wa Hermoniukianguka juu ya Mlima Sayuni.Kwa maana huko ndiko Mwenyezi Mungu alikoamuru baraka yake,naam, uzima hata milele.