Zaburi100
Dunia yote yaitwa kumsifu Mwenyezi Mungu
Zaburi ya shukrani.
1Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote.2Mwabuduni Mwenyezi Mungu kwa furaha;njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.3Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu.Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;sisi tu watu wake,kondoo wa malisho yake.4Ingieni malangoni mwake kwa shukranina katika nyua zake kwa kusifu,mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.5Kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwemana fadhili zake zadumu milele;uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.