Zaburi101swh_onmm
Ahadi ya kuishi kwa uadilifu na kwa haki
Zaburi ya Daudi.
1Nitaimba kuhusu upendo wako na haki yako;kwako wewe, Ee Mwenyezi Mungu, nitaimba sifa.2Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:utakuja kwangu lini?Nitatembea nyumbani mwangukwa moyo usio na lawama.3Sitaweka mbele ya macho yangukitu kiovu.Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani;hawatashikamana nami.4Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami;nitajitenga na kila ubaya.5Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri,huyo nitamnyamazisha;mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburihuyo sitamvumilia.6Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,ili waweze kuishi pamoja nami;yeye ambaye moyo wake hauna lawamaatanitumikia.7Mdanganyifu hatakaanyumbani mwangu,yeye asemaye kwa uongohatasimama mbele yangu.8Kila asubuhi nitawanyamazishawaovu wote katika nchi;nitamkatilia mbali kila mtenda maovukutoka mji wa Mwenyezi Mungu.