Nahumu1

1Neno la unabii kuhusu Ninawi. Kitabu cha maono cha Nahumu Mwelkoshi.

Hasira ya Mwenyezi Mungu dhidi ya Ninawi

2Mwenyezi Mungu ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi;Mwenyezi Mungu hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu.Mwenyezi Mungu hulipiza kisasi juu ya watesi wake,naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake.3Mwenyezi Mungu si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu,Mwenyezi Mungu hataacha kuadhibu wenye hatia.Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani,na mawingu ni vumbi la miguu yake.4Anakemea bahari na kuikausha,anafanya mito yote kukauka.Bashani na Karmeli zinanyaukana maua ya Lebanoni hukauka.5Milima hutikisika mbele yakena vilima huyeyuka.Nchi hutetemeka mbele yake,dunia na wote wanaoishi ndani yake.6Ni nani awezaye kuzuia hasira yake yenye uchungu?Nani awezaye kuvumilia hasira yake kali?Ghadhabu yake imemiminwa kama moto,na miamba inapasuka mbele zake.
7Mwenyezi Mungu ni Mwema,kimbilio wakati wa taabu.Huwatunza wale wanaomtegemea,8lakini kwa mafuriko makubwa,ataangamiza Ninawi;atafuatilia adui zake hadi gizani.
9Kila njama wanayopanga dhidi ya Mwenyezi Munguyeye atalikomesha;taabu haitatokea mara ya pili.10Watasongwa katikati ya miibana kulewa kwa mvinyo wao.Watateketezwa kama mabua makavu.11Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja,ambaye anapanga njamadhidi ya Mwenyezi Munguna kushauri uovu.
12Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:“Ingawa wana muungano nao ni wengi sana,watakatiliwa mbali na kuangamia.Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda,sitakutesa tena.13Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako,nami nitazivunjilia mbali pingu zako.”
14Hii ndiyo amri Mwenyezi Mungu aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi:“Hutakuwa na wazaowatakaoendeleza jina lako.Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kusubuzilizopo katika hekalu la miungu yenu.Nitaandaa kaburi lako,kwa maana wewe ni mwovu kabisa.”
15Tazama, huko juu milimani,miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema,ambaye anatangaza amani!Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako,nawe utimize nadhiri zako.Waovu hawatakuvamia tena;wataangamizwa kabisa.