1Taabu gani hii niliyo nayo!Nimefanana na yule akusanyayematunda ya kiangazi,aokotaye masazo baada ya kuvunwashamba la mizabibu;hakuna kishada chenye matunda ya kula,hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani.2Wanaomcha Mungu wameondolewa kutoka nchi;hakuna mtu mnyofu hata mmoja aliyebaki.Watu wote wanavizia kumwaga damu,kila mmoja anamwinda ndugu yake kwa wavu.3Mikono yote miwili ni hodari katika kufanya ubaya,mtawala anadai zawadi,hakimu anapokea rushwa,wenye nguvu wanaamuru wanachotaka:wote wanapanga njama pamoja.4Aliye mwema kupita wote kati yaoni kama mchongoma,anayeonekana mnyofu zaidi miongoni mwaoni mbaya kuliko uzio wa miiba.Siku ya walinzi wako imewadia,siku Mungu atakayokutembelea.Sasa ni wakati waowa kuchanganyikiwa.5Usimtumaini jirani;usiweke matumaini kwa rafiki.Hata kwa yule alalaye kifuani mwakouwe mwangalifu kwa maneno yako.6Kwa kuwa mwana humdharau baba yake,naye binti huinuka dhidi ya mama yake,mkwe kuwa kinyume na mama mkwe wake:adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa.7Lakini mimi, namtazama Mwenyezi Mungu kwa matumaini,namngoja Mungu Mwokozi wangu;Mungu wangu atanisikia mimi.
Israeli atainuka
8Usifurahie msiba wangu, ee adui yangu!Ingawa nimeanguka, nitainuka.Japo ninaketi gizani,Mwenyezi Mungu atakuwa nuru yangu.9Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake,nitabeba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu,hadi atakapotetea shauri languna kuithibitisha haki yangu.Atanileta nje kwenye mwanga,nami nitaiona haki yake.10Kisha adui yangu atalionanaye atafunikwa na aibu,yule aliyeniambia,“Yu wapi Mwenyezi Mungu, Mungu wako?”Macho yangu yataona kuanguka kwake,hata sasa atakanyagwa chini ya mguukama tope barabarani.11Siku ya kujenga kuta zako itawadia,siku ya kupanua mipaka yako.12Siku hiyo watu watakuja kwakokutoka Ashuru na miji ya Misri,hata kutoka Misri hadi Mto Frati,na kutoka bahari hadi bahari,na kutoka mlima hadi mlima.13Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake,kwa sababu ya matunda ya matendo yao.
Sala na sifa
14Wachunge watu wako kwa fimbo yako,kundi la urithi wako,ambalo linaishi peke yake msituni,katika maeneo ya malisho yenye rutuba.Waache walishe katika Bashani na Gileadikama ilivyokuwa siku za kale.15“Kama siku zile mlipotoka Misri,nitawaonesha maajabu yangu.”16Mataifa yataona na kuaibika,waliondolewa nguvu zao zote.Wataweka mikono yao kwenye vinywa vyaona masikio yao yatakuwa na uziwi.17Wataramba mavumbi kama nyoka,kama viumbe vinavyotambaa ardhini.Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka;watamgeukia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa hofunao watakuogopa.18Ni nani Mungu kama wewe,ambaye anaachilia dhambina kusamehe makosaya mabaki ya urithi wake?Wewe huwi na hasira milele,bali unafurahia kuonesha rehema.19Utatuhurumia tena,utazikanyaga dhambi zetuchini ya nyayo zako,na kutupa maovu yetu yotekatika vilindi vya bahari.20Utakuwa wa kweli kwa Yakobo,nawe utamwonesha Ibrahimu rehema,kama ulivyowaahidi kwa kiapo baba zetusiku za kale.