Yohana17
Isa ajiombea mwenyewe
1Baada ya Isa kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema:“Baba , saa imewadia. Mtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe.2Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa.3Nao uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe uliye Mungu wa pekee wa kweli, na Isa Al-Masihi uliyemtuma.4Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye.5Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujaumbwa.