Yohana16
1“Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani.2Watawatenga na masinagogi . Naam, saa yaja ambayo mtu yeyote atakayewaua atadhani kwa kufanya hivyo anamtumikia Mungu.3Nao watawatenda haya kwa sababu hawamjui Baba wala mimi.4Lakini nimewaambia ninyi mambo haya, ili saa hiyo ikiwadia mpate kukumbuka ya kuwa nilikuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.5“Sasa mimi ninaenda kwake yeye aliyenituma, lakini hakuna hata aniulizaye, ‘Unaenda wapi?’6Kwa sababu nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni.7Lakini nawaambia kweli, yafaa mimi niondoke, kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; lakini nikienda nitamtuma kwenu.8Naye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu.9Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;10kwa habari ya haki, kwa sababu ninaenda kwa Baba, nanyi hamtaniona tena;11kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.12“Bado ninayo mambo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili sasa.13Atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonesha mambo yajayo.14Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi.15Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu. Ndiyo maana nimesema Roho atachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi.”