1Neno la Mwenyezi Mungu lililomjia Sefania mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia, wakati wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda:
Onyo la maangamizi yanayokuja
2Mwenyezi Mungu asema,“Nitafagia kila kitukutoka uso wa dunia.3Nitafagilia mbali watu na wanyama;nitafagilia mbali ndege wa anganina samaki wa baharini.Wafanyao maovu watapata tu kokoto,nami nitamkatilia mbali mwanadamu atoke katika dunia,”asema Mwenyezi Mungu.
Dhidi ya Yuda
4“Nitaiadhibu Yudana wote wanaoishi Yerusalemu.Kutoka mahali hapa nitakatilia mbalikila mabaki ya Baali,majina ya wapagani na makuhaniwaabuduo sanamu:5wale ambao husujudu juu ya mapaakuabudu jeshi la vitu vya angani,wale ambao husujudu na kuapa kwa Mwenyezi Munguna ambao pia huapa kwa Malkamu,6wale wanaoacha kumfuata Mwenyezi Mungu,wala hawamtafuti Mwenyezi Munguwala kutaka shauri lake.7Nyamazeni mbele za Bwana Mungu Mwenyezi,kwa maana siku ya Mwenyezi Mungu iko karibu.Mwenyezi Mungu ameandaa dhabihu,amewaweka wakfu wale aliowaalika.8Katika siku ya dhabihu ya Mwenyezi Mungunitawaadhibu wakuuna wana wa mfalmena wale wote wanaovaanguo za kigeni.9Katika siku hiyo nitaadhibu wote ambaohukwepa kukanyaga kizingiti,ambao hujaza hekalu la miungu yaokwa dhuluma na udanganyifu.”10Mwenyezi Mungu asema, “Katika siku hiyokilio kitapanda juu kutoka lango la Samaki,maombolezo kutoka mtaa wa pili,na mshindo mkubwa kutoka vilimani.11Ombolezeni, ninyi mnaoishi katika eneo la sokoni;wafanyabiashara wenu wote wameangamizwa,wote ambao wanafanya biashara ya fedhawataangamizwa.12Wakati huo nitaupekua mji wa Yerusalemu kwa taa,na kuwaadhibu wale ambaowanakaa katika hali ya kuridhika,ambao ni kama divaiiliyobaki kwenye machicha,ambao hudhani, ‘Mwenyezi Mungu hatafanya lolote,jema au baya.’13Utajiri wao utatekwa nyara,nyumba zao zitabomolewa.Watajenga nyumba,lakini hawataishi ndani yake;watapanda mizabibulakini hawatakunywa divai yake.
Siku kubwa ya Mwenyezi Mungu
14“Siku kubwa ya Mwenyezi Mungu iko karibu:iko karibu na inakuja haraka.Sikilizeni! Kilio katika siku ya Mwenyezi Mungukitakuwa chungu.Shujaa atapiga ukelele wa vita huko.15Siku ile ni siku ya ghadhabu,siku ya fadhaa na dhiki,siku ya uharibifu na ukiwa,siku ya giza na utusitusi,siku ya mawingu na giza nene,16siku ya tarumbeta na kelele za vitadhidi ya miji yenye ngome,na dhidi ya minara mirefu.17Nitawaletea watu dhiki,nao watatembea kama vipofu,kwa sababu wametenda dhambidhidi ya Mwenyezi Mungu.Damu yao itamwagwa kama vumbina matumbo yao kama kinyesi.18Fedha yao wala dhahabu yaohazitaweza kuwaokoakatika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.Katika moto wa wivu wakedunia yote itateketezwa,kwa maana ghafula ataleta mwishowa wote wanaoishi duniani.”