Zekaria12swh_onmm
Adui za Yerusalemu kuangamizwa
1Neno la unabii: Hili ni neno la Mwenyezi Mungu kuhusu Israeli.Mwenyezi Mungu, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema:2“Nitaenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbisha mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.3Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza wenyewe.4Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye nitampiga kwa wazimu,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitalielekeza jicho langu la ulinzi juu ya nyumba ya Yuda, nami nitawapofusha farasi wote wa mataifa.5Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ni Mungu wao.’6“Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake.7“Mwenyezi Mungu atayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa kuliko ile ya Yuda.8Katika siku hiyo, Mwenyezi Mungu atawakinga wale wanaoishi Yerusalemu, ili aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa Mwenyezi Mungu akiwatangulia.9Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu.