Zekaria10swh_onmm

Mwenyezi Mungu ataitunza Yuda

1Mwombeni Mwenyezi Mungu mvua wakati wa vuli;ndiye Mwenyezi Mungu atengenezaye mawingu ya tufani.Huwapa watu manyunyu ya mvua,pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.2Sanamu huzungumza udanganyifu,waaguzi huona maono ya uongo;husimulia ndoto ambazo si za kweli,wanatoa faraja batili.Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoowalioteseka kwa kukosa mchungaji.
3“Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji,nami nitawaadhibu viongozi;kwa kuwa Mwenyezi Mungu,Mungu wa majeshi ya mbinguniatalichunga kundi lake,nyumba ya Yuda,naye atawafanya kama farasimwenye kiburi akiwa vitani.4Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni,kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema,kutoka kwake utatoka upinde wa vita,kutoka kwake atatoka kila mtawala.5Kwa pamoja watakuwa kama mashujaawanaokanyaga barabara za matopewakati wa vita.Kwa sababu Mwenyezi Mungu yu pamoja nao,watapigana na kuwashinda wapanda farasi.
6“Nitaiimarisha nyumba ya Yudana kuiokoa nyumba ya Yusufu.Nitawarejesha kwa sababunina huruma juu yao.Watakuwa kama watu ambaosijawahi kuwakataakwa sababu mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao,nami nitawajibu.7Waefraimu watakuwa kama mashujaa,mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai.Watoto wao wataona na kufurahi,mioyo yao itashangilia katika Mwenyezi Mungu.8Nitawaashiria na kuwakusanya ndani.Hakika nitawakomboa,nao watakuwa wengikama walivyokuwa mwanzoni.9Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa,hata hivyo wakiwa katika nchi za mbaliwatanikumbuka mimi.Wao na watoto wao watanusurika katika hatarinao watarudi.10Nitawarudisha kutoka Misrina kuwakusanya toka Ashuru.Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni,na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha.11Watapita katika bahari ya mateso;bahari iliyochafuka itatulizwana vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka.Kiburi cha Ashuru kitashushwa,nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.12Nitawaimarisha katika Mwenyezi Mungu,na katika jina lake watatembea,”asema Mwenyezi Mungu.