Tito1
Salamu
1Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Isa Al-Masihi kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu na kuijua kweli iletayo utauwa:2imani na ujuzi katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu, asiyesema uongo, aliahidi hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu,3naye kwa wakati wake aliouweka alilidhihirisha neno lake kupitia kwa mahubiri ambayo mimi nimewekewa amana kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu.4Kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tunayoshiriki sote.Neema na amani zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Mwokozi wetu, ziwe nawe.