Wimbo Ulio Bora8swh_onmm

1Laiti ungekuwa kwangu kama ndugu wa kiume,ambaye aliyanyonya matiti ya mama yangu!Kisha, kama ningekukuta huko nje,ningekubusu,wala hakuna mtu yeyote angenidharau.2Ningekuongoza na kukuletakatika nyumba ya mama yangu,yeye ambaye amenifundisha.Ningekupa divai iliyokolezwa unywe,asali ya maua ya mikomamanga yangu.3Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,na mkono wake wa kuume unanikumbatia.4Binti za Yerusalemu, ninawaagiza:msichochee wala kuamsha mapenzihata yatakapotaka yenyewe.
5Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikaniakimwegemea mpenzi wake?MpendwaNilikuamsha chini ya mtofaa,huko mama yako alipotunga mimba yako,huko yeye alipata uchungu akakuzaa.6Nitie kama muhuri moyoni mwako,kama muhuri kwenye mkono wako;kwa maana upendo una nguvu kama mauti,wivu wake ni mkatili kama Kuzimu .Unachoma kama mwali wa moto,kama mwali mkubwa wa moto wa Mwenyezi Mungu hasa.7Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,mito haiwezi kuugharikisha.Kama mtu angetoa mali yote ya nyumbani mwakekwa ajili ya upendo,angedharauliwa kabisa.8Tunaye dada mdogo,matiti yake hayajakua bado.Tutafanya nini kwa ajili ya dada yetuwakati atakapokuja kuposwa?9Kama yeye ni ukuta,tutajenga minara ya fedha juu yake.Na kama yeye ni mlango,tutamzungushia mbao za mwerezi.10Mimi ni ukuta,nayo matiti yangu ni kama minara.Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pakekama yule anayeleta utoshelevu.11Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni;alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji.Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yakeshekeli elfu moja za fedha.12Lakini shamba langu la mizabibuambalo ni langu mwenyeweni langu kutoa;hizo shekeli elfu moja ni kwa ajili yako, ee Sulemani,na shekeli mia mbili ni kwa ajiliya wale wanaotunza matunda yake.13Wewe ukaaye bustaninipamoja na rafiki mliohudhuria,hebu nisikie sauti yako!14Njoo, mpenzi wangu,uwe kama paaau kama ayala mchangajuu ya milima iliyojaa manukato.