Warumi1
Salamu
1Paulo, mtumishi wa Al-Masihi Isa, aliyeitwa kuwa mtume na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu,2Injili ambayo Mungu alitangulia kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika Maandiko Matakatifu,3yaani Injili inayomhusu Mwanawe, yeye ambaye kwa uzao wa mwili alikuwa mzao wa Daudi,4na ambaye kwa uwezo wa Roho wa utakatifu alidhihirishwa kuwa Mwana wa Mungu kwa ufufuo wake kutoka kwa wafu, yaani Isa Al-Masihi, Bwana wetu.5Kupitia kwake tumepokea neema na utume ili kuwaita watu wote wa mataifa waje kwenye utii utokanao na imani kwa ajili ya jina lake.6Ninyi nyote pia mko miongoni mwa watu walioitwa ili wapate kuwa mali ya Isa Al-Masihi.7Kwa wote walio Rumi wanaopendwa na Mungu na kuitwa kuwa watakatifu.Neema na amani zinazotoka kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi ziwe nanyi.