Zaburi95swh_onmm

Wimbo wa kumsifu Mwenyezi Mungu

1Njooni, tumwimbie Mwenyezi Mungu kwa furaha;tumfanyie kelele za shangweMwamba wa wokovu wetu.2Tuje mbele zake kwa shukrani,tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.
3Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu mkuu,mfalme mkuu juu ya miungu yote.4Mkononi mwake mna vilindi vya dunia,na vilele vya milima ni mali yake.5Bahari ni yake, kwani ndiye aliyeifanya,na mikono yake iliumba nchi kavu.
6Njooni, tusujudu, tumwabudu,tupige magoti mbele za Mwenyezi Mungu Muumba wetu,7kwa maana yeye ndiye Mungu wetu,na sisi ni watu wa malisho yake,kondoo chini ya utunzaji wake.Mkiisikia sauti yake leo,8msiifanye mioyo yenu migumukama mlivyofanya kule Meriba ,kama mlivyofanya siku ilekule Masa jangwani,9ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima,ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu.10Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile,nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka,nao hawajazijua njia zangu.”11Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu,“Kamwe hawataingia rahani mwangu.”