Zaburi93swh_onmm

Mwenyezi Mungu ni mkuu

1Mwenyezi Mungu anatawala, amejivika utukufu;Mwenyezi Mungu amejivika utukufutena amejivika nguvu.Dunia imewekwa imara,haitaondoshwa.2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;wewe umekuwa tangu milele.
3Bahari zimepaza, Ee Mwenyezi Mungu,bahari zimepaza sauti zake;bahari zimepaza sauti za mawimbi yake.4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:Mwenyezi Mungu aishiye juu sana ni mkuu.
5Ee Mwenyezi Mungu, sheria zako ni imara;utakatifu umepamba nyumba yakopasipo mwisho.