Zaburi87swh_onmm
Sifa za Yerusalemu
Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.
1Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;2Mwenyezi Mungu anayapenda malango ya Sayunikuliko makao yote ya Yakobo.3Mambo matukufu yanasemwa juu yako,ee mji wa Mungu:4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babelimiongoni mwa wale wanaonikubali mimi:Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,“Huyu na yule walizaliwa humo,naye Aliye Juu Sana mwenyeweatamwimarisha.”6Mwenyezi Mungu ataandika katika orodha ya mataifa:“Huyu alizaliwa Sayuni.”7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”