Zaburi84swh_onmm

Kuionea shauku nyumba ya Mwenyezi Mungu

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora.

1Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni,makao yako yapendeza kama nini!2Nafsi yangu inatamani sana,naam, hata kuona shauku,kwa ajili ya nyua za Mwenyezi Mungu;moyo wangu na mwili wanguvinamlilia Mungu Aliye Hai.
3Hata shomoro amejipatia makao,mbayuwayu amejipatia kiotamahali awezapo kuweka makinda yake:mahali karibu na madhabahu yako,Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni,Mfalme wangu na Mungu wangu.4Heri wale wanaokaa nyumbani mwako,wanaokusifu wewe daima.
5Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako,na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.6Wanapopita katika Bonde la Baka ,hulifanya mahali pa chemchemi,pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi .7Huendelea toka nguvu hadi nguvu,hadi kila mmoja afikapombele za Mungu huko Sayuni.
8Ee Bwana Mwenyezi Mungu,Mungu wa majeshi ya mbinguni,sikia maombi yangu;nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.9Ee Mungu, uitazame ngao yetu,mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.
10Siku moja katika nyua zako ni borakuliko siku elfu mahali pengine;afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangukuliko kukaa katika mahema ya waovu.11Kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu ni jua na ngao;Mwenyezi Mungu hutoa wema na heshima;hakuna kitu chema anachowanyimawale ambao hawana hatia.
12Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni,heri mtu anayekutumaini wewe.