Zaburi83swh_onmm
Maombi kwa ajili ya kushindwa kwa adui za Israeli
Wimbo. Zaburi ya Asafu.
1Ee Mungu, usikae kimya,usinyamaze, Ee Mungu, usikae mbali.2Tazama watesi wako wanafanya fujo,jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.3Kwa ujanja, wanapanga njama dhidi ya watu wako;wanapanga hila dhidi ya wale unaowapenda.4Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa,ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”5Kwa nia moja wanapanga njama pamoja,wanafanya muungano dhidi yako,6mahema ya Edomu na Waishmaeli,ya Wamoabu na Wahagari,7Gebali , Amoni na Amaleki,Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.8Hata Ashuru wameungana naokuwapa nguvu wazao wa Lutu.9Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani,na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabinihapo kijito cha Kishoni,10ambao waliangamia huko Endorina wakawa kama kinyesi juu ya ardhi.11Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu,watawala wao kama Zeba na Salmuna,12ambao walisema, “Na tumiliki maeneoya malisho ya Mungu.”13Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli,kama makapi yapeperushwayo na upepo.14Kama vile moto unavyoteketeza msituau mwali wa moto unavyounguza milima,15wafuatilie kwa tufani yakona kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.16Funika nyuso zao kwa aibuili watu walitafute jina lako, Ee Mwenyezi Mungu.17Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele,na waangamie kwa aibu.18Hebu wajue kuwa wewe, ambaye jina lako ni Mwenyezi Mungu,kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.