Zaburi82swh_onmm

Maombi kwa ajili ya kutaka haki

Zaburi ya Asafu.

1Mungu anaongoza kusanyiko kuu,anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:
2“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio hakina kuonesha upendeleo kwa waovu?3Teteeni wanyonge na yatima,tunzeni haki za maskini na waliodhulumiwa.4Mwokoeni mnyonge na mhitaji,wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.
5“Hawajui lolote, hawaelewi lolote.Wanatembea gizani;misingi yote ya dunia imetikisika.
6“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”;ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’7Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida;mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”
8Ee Mungu, inuka uihukumu nchi,kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.