Zaburi75swh_onmm
Mwenyezi Mungu ni mwamuzi
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu”. Zaburi ya Asafu. Wimbo.
1Ee Mungu, tunakushukuru,tunakushukuru wewe,kwa kuwa jina lako li karibu;watu husimulia matendo yako ya ajabu.2Unasema, “Ninachagua wakati maalum;ni mimi nihukumuye kwa haki.3Dunia inapotetemeka na watu wake wote,ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.4Kwa wale wenye majivuno ninasema,‘Msijisifu tena,’kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.5Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu;msiseme kwa kiburi.’ ”6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibiau kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.7Bali Mungu ndiye ahukumuye:Humshusha huyu na kumkweza mwingine.8Mkononi mwa Mwenyezi Mungu kuna kikombekilichojaa mvinyo unaotoka povuuliochanganywa na vikolezo;huumimina, nao waovu wote wa duniahunywa hata tone la mwisho.9Bali mimi, nitatangaza hili milele;nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.10Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote,bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.