Zaburi72swh_onmm
Maombi kwa ajili ya mfalme
Zaburi ya Sulemani.
1Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako,mwana wa mfalme kwa haki yako.2Atawaamua watu wako kwa haki,watu wako walioonewa kwa haki.3Milima italeta mafanikio kwa watu,vilima tunda la haki.4Atawatetea walioonewa miongoni mwa watuna atawaokoa watoto wa wahitaji,ataponda mdhalimu.5Atadumu kama jua linavyodumu, kama mwezi, vizazi vyote.6Atakuwa kama mvua inavyonyesha juu ya shamba lililofyekwa,kama manyunyu yanavyonyeshea ardhi.7Katika siku zake wenye haki watastawi;mafanikio yatakuwepo hadi mwezi utakapokoma.8Atatawala kutoka bahari hadi baharina kutoka Mto hadi miisho ya dunia.9Makabila ya jangwani watamsujudia,na adui zake wataramba mavumbi.10Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbaliwatamletea ushuru;wafalme wa Sheba na Sebawatampa zawadi.11Wafalme wote watamsujudiana mataifa yote yatamtumikia.12Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia,aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.13Atawahurumia wanyonge na wahitajina kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.14Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili,kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.15Aishi maisha marefu!Na apewe dhahabu ya Sheba.Watu wamwombee daimana kumbariki mchana kutwa.16Nafaka ijae tele katika nchi yote,juu ya vilele vya vilima na istawi.Tunda lake na listawi kama Lebanoni,listawi kama majani ya kondeni.17Jina lake na lidumu milele,na lidumu kama jua.Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake,nao watamwita aliyebarikiwa.18Ahimidiwe Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli,ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.19Jina lake tukufu lihimidiwe milele,ulimwengu wote ujae utukufu wake.Amen na Amen.20Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.