Zaburi70swh_onmm
Kuomba msaada
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi.
1Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;Ee Mwenyezi Mungu, njoo hima unisaidie.2Wale wanaotafuta kuniua,waaibishwe na kufadhaishwa;wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,warudishwe nyuma kwa aibu.3Wale wanaoniambia, “Aha! Aha!”na warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.4Lakini wote wanaokutafutawashangilie na kukufurahia,wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme,“Mwenyezi Mungu ni mkuu!”5Lakini mimi bado ni maskini na mhitaji;Ee Mungu, unijie haraka.Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;Ee Mwenyezi Mungu, usikawie.