Zaburi64swh_onmm
Kuomba ulinzi dhidi ya adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Ee Mungu, unisikie ninapoeleza lalamiko langu,uyahifadhi maisha yangu kutokana na vitisho vya adui.2Unifiche kutokana na njama za waovu,kutokana na fitina za kundi la watenda maovu.3Wananoa ndimi zao kama pangana kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha.4Hurusha mishale kutoka mavizio kwa mtu asiye na hatia,humrushia ghafula bila woga.5Kila mmoja humtia moyo mwenzakekatika mipango mibaya;huzungumza kuhusu kuficha mitego yao,nao husema, “Ni nani ataiona?”6Hupanga njama la dhuluma na kusema,“Tumebuni mpango mkamilifu!”Hakika nia na moyo wa mwanadamu vina hila.7Bali Mungu atawapiga kwa mishale,nao ghafula wataangushwa.8Atageuza ndimi zao wenyewe dhidi yaona kuwaleta kwenye maangamizi;wote wawaonao watatikisa vichwa vyaokwa dharau.9Wanadamu wote wataogopa,watatangaza kazi za Munguna kutafakari yale aliyoyatenda.10Wenye haki na wafurahi katika Mwenyezi Mungu,na wakimbilie kwake;wanyofu wote wa moyo na wamsifu yeye!