Zaburi63swh_onmm

Shauku kwa ajili ya uwepo wa Mwenyezi Mungu

Zaburi ya Daudi. Alipokuwa katika Jangwa la Yuda.

1Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu,nakutafuta kwa moyo wote;nafsi yangu inakuonea kiu,mwili wangu unakuonea wewe shauku,katika nchi kame na iliyochoka,mahali pasipo maji.
2Nimekuona katika mahali patakatifuna kuuona uwezo wako na utukufu wako.3Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai,midomo yangu itakuadhimisha.4Nitakusifu siku zote za maisha yangu,na kwa jina lako nitainua mikono yangu.5Nafsi yangu itatoshelezwa,kama kushiba vyakula vizuri;kwa midomo iimbayokinywa changu kitakusifu wewe.
6Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe;ninakuwaza makesha yote ya usiku.7Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu,chini ya uvuli wa mabawa yako naimba.8Nafsi yangu inaambatana nawe,mkono wako wa kuume hunishika.
9Wale wanaotafuta uhai wangu wataangamizwa;wataenda chini kwenye vilindi vya dunia.10Watatolewa wafe kwa upanga,nao watakuwa chakula cha mbweha.
11Bali mfalme atafurahi katika Mungu,wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu,bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.