Zaburi6swh_onmm
Sala ya kuomba msaada wakati wa taabu
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi.Zaburi ya Daudi.
1Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako,wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.2Unirehemu Mwenyezi Mungu,kwa maana nimedhoofika;Ee Mwenyezi Mungu, uniponye,kwa maana mifupa yanguina maumivu makali.3Nafsi yangu ina uchungu mwingi.Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu, hadi lini?4Geuka, Ee Mwenyezi Mungu, unikomboe,uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.5Hakuna mtu anayekukumbukaakiwa amekufa.Ni nani awezaye kukusifuakiwa Kuzimu ?6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;usiku kucha natiririshakitanda changu kwa machozi;nimelowesha kiti changukwa machozi yangu.7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,kwa maana Mwenyezi Mungu amesikia kulia kwangu.9Mwenyezi Mungu amesikia kilio changu kwa huruma,Mwenyezi Mungu amekubali sala yangu.10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,watarudi nyuma na waaibishwe kwa ghafula.