Zaburi52swh_onmm
Hukumu ya Mwenyezi Mungu
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi. Baada ya Doegi, Mwedomu kumwendea Sauli na kumjulisha kuwa: “Daudi ameenda nyumbani mwa Ahimeleki.”
1Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya?Kwa nini unajivuna mchana kutwa,wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu?2Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi.Ni kama wembe mkali, ninyi mnaofanya hila.3Unapenda mabaya kuliko mema,uongo kuliko kusema kweli.4Unapenda kila neno lenye kudhuru,ewe ulimi wenye hila!5Hakika Mungu atakushusha chinikwa maangamizi ya milele:atakunyakua na kukuondoa kwa nguvukutoka hema lako,atakung’oa kutoka nchi ya walio hai.6Wenye haki wataona na kuogopa;watamcheka, wakisema,7“Huyu ni yule mtu ambayehakumfanya Mungu kuwa ngome yake,bali alitumainia wingi wa utajiri wake,na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”