Zaburi48swh_onmm
Sayuni, mji wa Mwenyezi Mungu
Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora.
1Mwenyezi Mungu ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana,katika mji wa Mungu wetu,mlima wake mtakatifu.2Ni mzuri katika kuinuka juu kwake,furaha ya dunia yote.Kama vilele vya juu vya Safoni ni Mlima Sayuni,mji wa Mfalme Mkuu.3Mungu yuko katika ngome zake;amejionesha mwenyewe kuwa ngome yake.4Wafalme walipounganisha nguvu,waliposonga mbele pamoja,5walimwona, wakashangaa,wakakimbia kwa hofu.6Kutetemeka kuliwashika huko,maumivu kama ya mwanamkemwenye uchungu wa kuzaa.7Uliwaangamiza kama meli za Tarshishizilizovunjwa na upepo wa mashariki.8Kama tulivyokuwa tumesikia,ndivyo tulivyoonakatika mji wa Mwenyezi Mungu,Mungu wa majeshi ya mbinguni,katika mji wa Mungu wetu:Mungu ataufanya uwe salama milele.9Ee Mungu, hekaluni mwakotunatafakari upendo wako usiokoma.10Ee Mungu, kama jina lako lilivyo,sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia,mkono wako wa kuume umejazwa na haki.11Mlima Sayuni unashangilia,vijiji vya Yuda vinafurahikwa sababu ya hukumu zako.12Tembeeni katika Sayuni,uzungukeni mji,hesabuni minara yake;13yatafakarini vyema maboma yake,angalieni ngome zake,ili mpate kusimulia habari zakekwa kizazi kijacho.14Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele;atakuwa kiongozi wetu hata mwisho.