Zaburi42swh_onmm
Maombi ya mtu aliye uhamishoni
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora.
1Kama ayala anavyoonea shauku vijito vya maji,ndivyo nafsi yangu inavyokuonea shauku, Ee Mungu.2Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai.Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu?3Machozi yangu yamekuwa chakula changuusiku na mchana,huku watu wakiniambia mchana kutwa,“Yuko wapi Mungu wako?”4Mambo haya nayakumbukaninapoimimina nafsi yangu:Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu,nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu,kwa kelele za shangwe na za shukranikatikati ya umati wa watu waliosherehekea.5Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?Weka tumaini lako kwa Mungu,kwa kuwa bado nitamsifu,Mwokozi wangu na Mungu wangu.6Nafsi yangu inasononeka ndani yangu;kwa hiyo nitakukumbukakutoka nchi ya Yordani,katika vilele vya Hermoni,kutoka Mlima Mizari.7Kilindi huita kilindi,katika ngurumo za maporomoko ya maji yako;mawimbi yako yote pamoja na viwimbivimepita juu yangu.8Mwenyezi Mungu huelekeza upendo wake mchana,wimbo wake uko nami usiku:maombi kwa Mungu wa uzima wangu.9Ninamwambia Mungu Mwamba wangu,“Kwa nini umenisahau?Kwa nini niendelee kuomboleza,nikiteswa na adui?”10Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makaliadui zangu wanaponidhihaki,wakiniambia mchana kutwa,“Yuko wapi Mungu wako?”11Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?Weka tumaini lako kwa Mungu,kwa kuwa bado nitamsifu,Mwokozi wangu na Mungu wangu.