Zaburi4swh_onmm
Sala ya jioni ya kuomba msaada
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Daudi.
1Nijibu nikuitapo,Ee Mungu wangu mwenye haki!Nipumzishe katika shida zangu;nirehemu, usikie ombi langu.2Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangukuwa aibu hadi lini?Mtapenda udanganyifuna kufuata miungu ya uongo hadi lini?3Fahamuni hakika kwamba Mwenyezi Mungu amewatengawale wamchao kwa ajili yake;Mwenyezi Mungu atanisikia nimwitapo.4Katika hasira yako, usitende dhambi.Tulieni kimya mkiwa vitandani mwenu,mkiichunguza mioyo yenu.5Toeni dhabihu zilizo haki;mtegemeeni Mwenyezi Mungu.6Wengi wanauliza, “Ni nani awezayekutuonesha jema lolote?”Ee Mwenyezi Mungu, tuangazie nuru ya uso wako.7Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwakuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.8Nitajilaza chini na kulala kwa amani,kwa kuwa wewe peke yako, Ee Mwenyezi Mungu,waniwezesha kukaa kwa salama.