Zaburi38

Maombi ya mtu anayeteseka

Zaburi ya Daudi. Maombi.

1Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako,wala kuniadhibu katika ghadhabu yako.2Kwa kuwa mishale yako imenichoma,na mkono wako umenipiga.3Hakuna afya mwilini mwangukwa sababu ya ghadhabu yako,mifupa yangu haina uzimakwa sababu ya dhambi zangu.4Maovu yangu yamenifunikakama mzigo mzito mno.
5Majeraha yangu yameoza na yananuka,kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.6Nimeinamishwa chini na kushushwa sana,mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.7Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo,hakuna afya mwilini mwangu.8Nimedhoofika na kupondwa kabisa,nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni.
9Ee Bwana, yote ninayoyaonea shaukuyako wazi mbele zako,kutamani kwangu sanahakufichiki mbele zako.10Moyo wangu unapigapiga,nguvu zangu zimeniishia;hata macho yangu yametiwa giza.11Rafiki na wenzangu wananikwepakwa sababu ya majeraha yangu;majirani wangu wanakaa mbali nami.12Wale wanaotafuta uhai wanguwanatega mitego yao,wale ambao wangetaka kunidhuruhuongea kuhusu maangamizi yangu;hupanga hila mchana kutwa.
13Mimi ni kama kiziwi, asiyeweza kusikia,ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake;14nimekuwa kama mtu asiyesikia,ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu.15Ee Mwenyezi Mungu, ninakungojea wewe,Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, utajibu.16Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie,wala wajitukuze juu yangumguu wangu unapoteleza.”
17Kwa maana ninakaribia kuanguka,na maumivu yangu yananiandama siku zote.18Naungama uovu wangu,ninataabishwa na dhambi yangu.19Wengi wamekua adui zangu bila sababu;wale wanaonichukia bure ni wengi.20Wanaolipa wema wangu kwa maovuhunisingizia ninapofuata lililo jema.
21Ee Mwenyezi Mungu, usiniache,usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu.22Ee Bwana Mwokozi wangu,uje upesi kunisaidia.