Zaburi36swh_onmm
Uovu wa mwanadamu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Mwenyezi Mungu.
1Kuna neno moyoni mwangukutoka kwa Mungukuhusu hali ya dhambi ya mwovu.Hakuna hofu ya Mungumbele ya macho yake.2Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mnohata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake.3Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu,ameacha kuwa mwenye hekima au kutenda mema.4Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya,hujitia katika njia ya dhambina hakatai lililo baya.5Upendo wako, Ee Mwenyezi Mungu, unafika hadi mbinguni,uaminifu wako hadi kwenye anga.6Haki yako ni kama milima mikubwa,hukumu zako ni kama kilindi kikuu.Ee Mwenyezi Mungu, wewe huwahifadhimwanadamu na mnyama.7Upendo wako usiokomani wa thamani mno!Watu wakuu na wadogohujificha uvulini wa mabawa yako.8Wanajifurahisha katika wingi ulio nyumbani mwako,nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako.9Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima,katika nuru yako twaona nuru.10Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe,haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo.11Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu,wala mkono wa mwovu usinifukuze.12Tazama jinsi watenda maovu walivyoanguka:wametupwa chini, hawawezi kuinuka!