Zaburi32swh_onmm
Furaha ya msamaha
Zaburi ya Daudi. Funzo.
1Heri mtu aliyesamehewa makosa yake,ambaye dhambi zake zimefunikwa.2Heri mtu yule ambaye Mwenyezi Munguhamhesabii dhambi,na ambaye rohoni mwakehamna udanganyifu.3Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaakwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.4Usiku na mchanamkono wako ulinilemea,nguvu zangu zilinyonywakama vile katika joto la kiangazi.5Kisha nikakiri dhambi yangu kwako,wala sikuficha uovu wangu.Nilisema, “Nitaungamamakosa yangu kwa Mwenyezi Mungu.”Ndipo uliponisamehehatia ya dhambi yangu.6Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombewakati unapopatikana,hakika maji makuu yatakapofurikahayatamfikia yeye.7Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha,utaniepusha na taabuna kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.8Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea;nitakushauri na kukuangalia.9Usiwe kama farasi au nyumbuwasio na akili,ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamula sivyo hawatakukaribia.10Mtu mwovu ana taabu nyingi,bali upendo usio na kikomo wa Mwenyezi Munguunamzunguka mtu anayemtumaini.11Shangilieni katika Mwenyezi Mungu na mfurahi, enyi wenye haki!Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo!