Zaburi30swh_onmm
Maombi ya shukrani
Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi.
1Nitakutukuza wewe, Ee Mwenyezi Mungu,kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,na hukuacha adui zanguwashangilie juu yangu.2Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nilikuita unisaidiena wewe umeniponya.3Ee Mwenyezi Mungu, umenitoa Kuzimu ,umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.4Mwimbieni Mwenyezi Mungu, enyi watakatifu wake;lisifuni jina lake takatifu.5Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,bali upendo wake hudumu siku zote.Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,lakini furaha huja asubuhi.6Nilipofanikiwa nilisema,“Sitatikiswa kamwe.”7Ee Mwenyezi Mungu, uliponijalia,uliuimarisha mlima wangu,lakini ulipouficha uso wakonilifadhaika.8Kwako wewe, Ee Mwenyezi Mungu, niliita,niliomba rehema kwa Bwana:9“Kuna faida gani katika kuangamia kwangu,katika kushuka kwangu shimoni?Je, mavumbi yatakusifu?Je, yatatangaza uaminifu wako?10Ee Mwenyezi Mungu, unisikie na kunihurumia;Ee Mwenyezi Mungu, uwe msaada wangu.”11Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza,ulinivua gunia ukanivika shangwe,12ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya.Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nitakushukuru milele.