Zaburi29swh_onmm

Sauti ya Mwenyezi Mungu wakati wa dhoruba

Zaburi ya Daudi.

1Mpeni Mwenyezi Mungu, enyi mashujaa,mpeni Mwenyezi Mungu utukufu na nguvu.2Mpeni Mwenyezi Mungu utukufu unaostahili jina lake;mwabuduni Mwenyezi Mungu katika uzuri wa utakatifu wake.3Sauti ya Mwenyezi Mungu iko juu ya maji;Mungu wa utukufu hupiga radi,Mwenyezi Mungu hupiga radi juu ya maji makuu.
4Sauti ya Mwenyezi Mungu ina nguvu;sauti ya Mwenyezi Mungu ni tukufu.5Sauti ya Mwenyezi Mungu huvunja mierezi;Mwenyezi Mungu huvunja vipande vipandemierezi ya Lebanoni.6Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,Sirioni urukaruke kama mwana nyati.7Sauti ya Mwenyezi Mungu hupigakwa miali ya radi.8Sauti ya Mwenyezi Mungu hutikisa jangwa;Mwenyezi Mungu hutikisa Jangwa la Kadeshi.9Sauti ya Mwenyezi Mungu huzalisha ayala,na huuacha msitu wazi.Hekaluni mwake wote wasema,“Utukufu!”
10Mwenyezi Mungu huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika;Mwenyezi Mungu ametawazwa kuwa Mfalme milele.11Mwenyezi Mungu huwapa watu wake nguvu;Mwenyezi Mungu huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.