Zaburi28swh_onmm

Kuomba msaada

Zaburi ya Daudi.

1Ninakuita wewe, Ee Mwenyezi Mungu, Mwamba wangu;usikatae kunisikiliza.Kwa sababu ukinyamazanitafanana na walioshuka shimoni.2Sikia kilio changu nikikuomba unihurumie,ninapokuita ili unisaidie,ninapoinua mikono yangu kuelekeaPatakatifu pa Patakatifu pako.
3Usiniburute pamoja na waovu,pamoja na hao watendao mabaya,ambao huzungumza na majirani zao maneno mazuri,lakini mioyoni mwao wameficha chuki.4Walipe sawasawa na matendo yao,sawasawa na matendo yao maovu;walipe sawasawa na kazi za mikono yao,uwalipe wanavyostahili.5Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Mwenyezi Mungu,na yale ambayo mikono yake imetenda,atawabomoa na kamwehatawajenga tena.
6Ahimidiwe Mwenyezi Mungu,kwa maana amesikia kilio changunikimwomba anihurumie.7Mwenyezi Mungu ni nguvu zangu na ngao yangu,moyo wangu umemtumaini yeye,nami nimesaidiwa.Moyo wangu unarukaruka kwa furahanami nitamshukuru kwa wimbo.
8Mwenyezi Mungu ni nguvu ya watu wake,ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.9Waokoe watu wako na uubariki urithi wako;uwe mchungaji wao na uwabebe milele.