Zaburi26swh_onmm
Maombi ya mtu mwema
Zaburi ya Daudi.
1Ee Mwenyezi Mungu, nithibitishe katika haki,maana nimeishi maisha yasiyo na lawama;nimemtumainia Mwenyezi Mungubila kusitasita.2Ee Mwenyezi Mungu, unijaribu, unipime,uuchunguze moyo wanguna mawazo yangu;3kwa maana upendo wakouko mbele yangu daima,nami natembea siku zotekatika kweli yako.4Siketi pamoja na watu wadanganyifu,wala siandamani na wanafiki,5ninachukia kusanyiko la watenda maovu,na ninakataa kuketi pamoja na waovu.6Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia,naikaribia madhabahu yako, Ee Mwenyezi Mungu,7nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa,huku nikisimulia matendo yako ya ajabu.8Ee Mwenyezi Mungu, naipenda nyumba yako unakoishi,mahali pale utukufu wako hukaa.9Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi,wala uhai wangu pamoja na wanaomwaga damu,10ambao mikononi mwao kuna mipango miovu,ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa.11Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama;nikomboe na unihurumie.12Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare;katika kusanyiko kuu nitamsifu Mwenyezi Mungu.