Zaburi22swh_onmm

Kilio cha uchungu na wimbo wa sifa

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Kulungu wa Alfajiri”. Zaburi ya Daudi.

1Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa?Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu?2Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu,hata usiku, sinyamazi.
3Hata hivyo umesimikwa kwenye kiti cha enzi,Wewe Uliye Mtakatifu;wewe ni sifa ya Israeli.4Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao,walikutumaini nawe ukawaokoa.5Walikulilia wewe na ukawaokoa,walikutegemea wewe nao hawakuaibika.
6Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu,wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau.7Wote wanaoniona wananidhihaki;wananivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao:8Wanasema, “Amtegemea Mwenyezi Mungu,basi Mwenyezi Mungu na amwokoe.Amkomboe basi, kwa maanaanapendezwa naye.”
9Hata hivyo ulinitoa tumboni,ukanifanya nikutegemee,hata nilipokuwa ninanyonyamatiti ya mama yangu.10Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa,toka tumboni mwa mama yanguumekuwa Mungu wangu.11Usiwe mbali nami,kwa maana shida iko karibuna hakuna wa kunisaidia.
12Mafahali wengi wamenizunguka,mafahali wa Bashani wenye nguvuwamenizingira.13Simba wanaonguruma na kurarua mawindowanapanua vinywa vyao dhidi yangu.14Nimemiminwa kama maji,mifupa yangu yote imeteguka viungoni.Moyo wangu umegeuka kuwa nta,umeyeyuka ndani yangu.15Nguvu zangu zimekauka kama kigae,ulimi wangu umegandamanana kaakaa la kinywa changu,kwa sababu umenilazakatika mavumbi ya kifo.16Mbwa wamenizunguka,kundi la watu waovu limenizingira;wamenidunga mikono na miguu.17Naweza kuhesabu mifupa yangu yote,watu wananikodolea macho na kunisimanga.18Wanagawana nguo zangu,na vazi langu wanalipigia kura.
19Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu,usiwe mbali.Ee Nguvu yangu,uje haraka unisaidie.20Okoa maisha yangu na upanga,uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa.21Niokoe kutoka kinywani mwa simba,niokoe kutoka pembe za nyati.
22Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu,katika kusanyiko nitakusifu wewe.23Ninyi ambao mnamcha Mwenyezi Mungu, msifuni!Ninyi nyote wazao wa Yakobo, mheshimuni yeye!Mcheni yeye, ninyi wazao wa Israeli!24Kwa maana hakupuuza wala kudharaumateso ya aliyeteswa;hakumficha uso wakebali alisikiliza kilio chake.
25Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa,nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wanaokucha wewe.26Maskini watakula na kushiba,wale wanaomtafuta Mwenyezi Mungu watamsifu:mioyo yenu na iishi milele!27Miisho yote ya dunia itakumbukana kumgeukia Mwenyezi Mungu,nazo jamaa zote za mataifazitasujudu mbele zake,28kwa maana ufalme ni wa Mwenyezi Mungunaye huyatawala mataifa.
29Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu.Wote wanaoshuka mavumbiniwatapiga magoti mbele yake,wote ambao hawawezikudumisha uhai wao.30Wazao wa baadaye watamtumikia yeye;vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana.31Watatangaza haki yake kwa watuambao hawajazaliwa bado,kwa maana yeye ametenda hili.