Zaburi21swh_onmm
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya ushindi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Ee Mwenyezi Mungu, mfalme huzifurahia nguvu zako.Tazama jinsi furaha yake ilivyo kuukwa ushindi unaompa!2Umempa haja ya moyo wakena hukumzuilia maombi ya midomo yake.3Ulimkaribisha kwa baraka telena kumvika taji la dhahabu safi kichwani pake.4Alikuomba maisha, nawe ukampa,wingi wa siku milele na milele.5Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa,umeweka juu yake fahari na utukufu.6Hakika umempa baraka za milele,umemfanya awe na furahakwa shangwe ya uwepo wako.7Kwa kuwa mfalme anamtumaini Mwenyezi Mungu;kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.8Mkono wako utawashika adui zako wote,mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.9Wakati utajitokeza,utawafanya kama tanuru la moto.Katika ghadhabu yake Mwenyezi Mungu atawameza,moto wake utawateketeza.10Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani,uzao wao kutoka wanadamu.11Ingawa watapanga mabaya dhidi yakona kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,12kwa kuwa utawafanya wakimbieutakapowalenga usoni paokwa mshale kutoka upinde wako.13Ee Mwenyezi Mungu, utukuzwe katika nguvu zako,tutaimba na kusifu nguvu zako.