Zaburi2swh_onmm
Mfalme aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu
1Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya,na makabila ya watu kula njama bure?2Wafalme wa dunia wanajipangana watawala wanajikusanyadhidi ya Mwenyezi Munguna dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.3Wanasema, “Tuvunje minyororo yaona kuvitupilia mbali vifungo vyao.”4Yeye anayetawala mbinguni hucheka,Bwana huwadharau.5Kisha huwakemea katika hasira yakena kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,6“Nimemtawaza Mfalme wangujuu ya Sayuni,mlima wangu mtakatifu.”Ushindi wa mfalme
7Nitatangaza amri ya Mwenyezi Mungu:Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu;leo mimi nimekuwa Baba yako.8Niombe, nami nitayafanya mataifakuwa urithi wako,na miisho ya dunia kuwa milki yako.9Utawapondaponda kwa fimbo ya chuma,na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”10Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima;mwonyeke, enyi watawala wa dunia.11Mtumikieni Mwenyezi Mungu kwa hofuna mshangilie kwa kutetemeka.12Mbusu Mwana, asije akakasirikanawe ukaangamizwa katika njia yako,kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula.Heri wote wanaomkimbilia.