1Msifuni Mwenyezi Mungu!Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi Mungu,2Nitamsifu Mwenyezi Mungu maisha yangu yote;nitamwimbia Mungu wangu sifawakati wote ningali hai.3Usiweke tumaini lako kwa wakuu,kwa wanadamu ambao hufa,ambao hawawezi kuokoa.4Roho yao itokapo hurudi mavumbini,siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.5Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,ambaye tumaini lake ni katika Mwenyezi Mungu, Mungu wake,6Muumba wa mbingu na nchi,na bahari na vyote vilivyomo:Mwenyezi Mungu anayedumu kuwa mwaminifumilele na milele.7Naye huwapatia haki waliodhulumiwa,na kuwapa wenye njaa chakula.Mwenyezi Mungu huwaweka wafungwa huru,8Mwenyezi Mungu huwafumbua vipofu macho,Mwenyezi Mungu huwainua waliolemewa na mizigo yao,Mwenyezi Mungu huwapenda wenye haki.9Mwenyezi Mungu huwalinda wagenina kuwategemeza yatima na wajane,lakini hupinga njia za waovu.10Mwenyezi Mungu atamiliki milele,Mungu wako, ee Sayuni,kwa vizazi vyote.Msifuni Mwenyezi Mungu.