Zaburi131swh_onmm
Kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.
1Moyo wangu hauna kiburi, Ee Mwenyezi Mungu,macho yangu hayajivuni;sijishughulishi na mambo makuu kunizidiwala mambo ya ajabu mno kwangu.2Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu;kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake,kama mtoto aliyeachishwa kunyonyandivyo ilivyo nafsi iliyo ndani yangu.3Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungutangu sasa na hata milele.