Zaburi129swh_onmm

Maombi dhidi ya adui za Israeli

Wimbo wa kwenda juu.

1Wamenitesa sana tangu ujana wangu;Israeli na aseme sasa:2wamenitesa sana tangu ujana wangu,lakini bado hawajanishinda.3Wakulima wamelima mgongo wangu,na kufanya mifereji yao mirefu.4Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki;amenifungua toka kamba za waovu.
5Wale wote wanaoichukia Sayunina warudishwe nyuma kwa aibu.6Wawe kama majani juu ya paa,ambayo hunyauka kabla hayajakua;7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,wala akusanyaye kujaza mikono yake.8Wale wapitao karibu na wasiseme,“Baraka ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako;tunakubariki katika jina la Mwenyezi Mungu.”